KOCHA Gerardo Martino amepewa
mkataba wa miaka miwili kuinoa Barcelona akichukua nafasi ya Tito Vilanova aliyejiuzulu
kwa sababu za kiafya.
Martino maarufu kama Tata,
ametua Camp Nou kwa ushawishi mkubwa wa Mkurugenzi wa Michezo wa klabu hiyo, Andoni
Zubizarreta aliyezungumza naye kabla ya jana kutangazwa rasmi.
Tata aliondoka Hispania tangu
juzi kwenda Hispania kwa mazungumzo kabla ya kusaini mkataba kubeba mikoba ya Vilanova
aliyejiuzulu Ijumaa iliyopita kujipa muda zaidi wa kupigania afya yake.
Vilanova aliyekuwa amechukua
nafasi ya Pep Guardiola mwaka mmoja uliopita, amekuwa akisumbuliwa na maradhi
ya kansa ya koo ambapo mara kadhaa amekuwa akitibiwa na kupata nafuu ya muda.
Tata (50), atasaidiwa na kocha
wa viungo, Elvio Paolorroso na Kocha Msaidizi, Jorge Pautasso, ametwaa nafasi
hiyo akimpiku kiungo wa zamani wa timu hiyo, Luis Enrique aliyekuwa
akitajwa.
Martino ni Muargentina wa nne
kuinoa Barcelona, akitanguliwa na Helenio Herrera, Roque Olsen na Cesar Luis Menotti.
Nje ya ukocha, Enrique
ataungana na Muargentina mwenzake, Lionel Messi nyota mahiri katika kikosi
hicho ambacho kitaingia kwenye msimu mpya wa La Liga kama bingwa mtetezi.
Jumatatu hii Messi alizungumza
na Tata aliyewahi kuinoa Newell na Paraguay na kaka yake Matias Messi na kumpongeza Martino kwa jukumu jipya Camp Nou.
"Karibu Tata!!" aliandika
Messi kupitia Twitter. " Naamini utaendelea kupata mafanikio ukiwa hapa!! Asante Tito!! Mungu akubariki!!"
No comments:
Post a Comment