Sunday, October 13, 2013

Ujerumani, Ubelgiji, Uswisi zatwaa tiketi

Ujerumani, Ubelgiji, Uswisi zatwaa tiketi
Ozil ndani ya nyumba

TIMU za Ujeruamni, Ubeljigi na Uswisi, juzi usiku zilijitwalia tiketi ya Kombe la Dunia za mwakani nchini Brazil kutoka bara la Ulaya ambalo litatoa jumla ya timu 12.

Wakati maimba hiyo ikitangulia, bingwa mtetezi Hispania chini ya kocha wake Vicente Del Bosque, England na Russia, zinasubiri majaaliwa yao katika mechi za mwisho, Oktoba 15.
Ujerumani imejitwalia tiketi yake baada ya juzi kuifunga  Ireland 3-0 huku Ubelgiji ikiichapa Croatia 2-1 na Uswisi kuichakaza Albania 2-1.
Miamba hiyo imeungana na mingine kama Italia na Uholanzi iliyotangulia kupata tiketi ya Brazil.
Akizungumzia mafanikio ya Ubelgiji, kiungo Marouane Fellaini alisema wanapaswa kujivunia kiwango cha timu yao kwani pamoja na ugumu wa kampeni hiyo, wamefanikiwa.
Nazo England, Hispania na Russia zilishinda na kuongoza makundi yao, japo zinasubiri kupata matokeo mazuri katika mechi hizo za mwisho.
Kinara katika makundi tisa ya Ulaya, atajitwalia tiketi ya Brazil huku nane zitakazomaliza nafasi ya pili, zitachuana hatua ya mtoano kuwania nafasi nne kufikia 12 kwa Ulaya.
Mabao ya Ujerumani yalifungwa na Sami Khedira, Andre Schuerrle na Mesut Ozil, nyota wa Arsenal ya England aliyetokea Real Madrid ya Hispania.
Ujerumani imekata tiketi ya Kombe la Dunuia ikitokea kundi C, itacheza fainali hizo mara ya 18 tangu kuasisiwa kwake mwaka 1930.
Katika mechi nyingine, bao la dakika ya 86 likifungwa na Zlatan Ibrahimovic, liliipa Sweden ushindi wa 2-1 dhidi ya Austria, ikiwa nafasi ya pili huku Faroe Islands ikitoka sare ya 1-1 dhidi ya Kazakhstan.
Wachezaji wa Ubelgiji wakishangilia baada ya kufuzu Kombe la Dunia
Mbao mawili ya Romelu Lukaku, yaliipa Ubelgiji pointi tatu hivyo kuongoza kundi A, hivyo kuikwaa tiketi ya fainali za Kombe la Dunia mara ya kwanza tangu 2002 huku  Croatia ya pili.
Nayo Wales juzi ilishinda 1-0 dhidi ya Macedonia 1-0 katika mechi nyingine ya kundi hilo.
Aidha, mabao ya Xherdan Shaqiri na Michael Lang yaliipa ushindi Uswisi na kukamata usukani wa kundi E, hivyo kujitwalia tiketi ya Brazil huku Iceland iliyoichapa Cyprus 2-0, imebaki nafasi ya pili, mbele pointi moja dhidi ya  Slovenia iliyoichapa Norway 3-0.
Nayo England, juzi ilishinda 4-1 dhidi ya Montenegro 4-1 mjini London, hivyo kuongoza kwa tofauti ya pointi moja dhidi ya Ukraine, iliyoifunga Poland 1-0 katika kundi H.
England inahitaji ushindi katika mechi ya mwisho dhidi ya Poland hapo Oktoba 15, kutwaa tiketi huku Ukraine ikimaliza na San Marino, iliyofungwa 3-0  na Moldova.
England ilitangulia kupata bao dakika ya 49, likifungwa na Wayne Rooney kabla ya Branko Boskovic wa Montenegro kujifunga, likiwa la pili kwa England.
Hata hivyo, Dejan Damjanovic aliifungia Montenegro bao, lakini bao la Andros Townsend na Daniel Sturridge, yaliipa England ushindi wa mabao 4-1.
Raha ya ushindi
Katika kundi I, mabingwa wa Dunia Hispania waliwafunga Belarus 2-1 na kukamata usukani wa kundi mbele ya Ufaransa.
Mashuti ya Xavi Hernandez na Alvaro Negredo, ndio yalipeleka kilio kwa Belarus, hivyo sasa kuhityaji walau sare tu kutoka kwa Georgia kujitwalia tiketi ya Brazil.
Nayo Russia iliitandika Luxembourg 4-0, hivyo kukamata usukani wa kundi F, mbele ya Ureno iliyotoka sare ya 1-1 dhidi ya Israel huku Azerbaijan ikishinda 2-0 dhidi ya  Ireland Kaskazini.
Bosnia-Herzegovina iliichapa Liechtenstein 4-1, huku Ugiriki ikiifunga Slovakia 1-0, hivyo kukabana katika kundi G, wakiwa na pointi 22. Lithuania imeifunga Latvia 2-0.

Mtoano
Uturuki na Romania zimejiweka kwenye mazingira ya kucheza hatua ya mtoano wa timu nane kuania nafasi nne kutokana na kufungana kwa pointi katika kundi D, mbele ya Hungary iliyochapwa 8-1 na Uholanzi.
Hiyo ni baada ya Uturuki kushinda 2-0 dhidi ya Estonia 2 huku Romania ikishinda 4-0 dhidi ya Andorra.
Timu nne za kundi B, zimebaki kupigania kucheza hatua ya mtoano baada ya Italia kuvuna sare ya 2-2 dhidi ya  Denmark.
Denmark na Bulgaria, zilizofungwa 2-1 dhidi ya Armenia, zinafungana kwa pointi 13 kila moja huku Armenia na Czech iliyoshinda 3-1 dhidi ya Malta, zikiwa na pointi 12ts.

Zenye tiketi ya Brazil
Ukimwondoa mwenye Brazil mwenye tiketi ya moja kwa moja, nyingine ni Argentina, Australia, Ubelgiji, Costa Rica, Ujerumani, Iran, Italia, Japan, Uholanzi, Korea Kusini, Uswisi na Marekani.

No comments:

Post a Comment