BRAZIL chini ya Kocha wake Luiz Felipe Scolari, jana iliichapa Korea Kusini katika mechi ya kirafiki ya kimataifa, ukiwa ni ushindi wa tatu mfululizo kabla ya kuikabili Zambia, Jumanne ijayo katika mechi nyingine ya kimataifa.
Mabao ya wenyeji hao wa fainali za Kombe la Dunia za mwakani, yalifungwa na Neymar na Oscar.
Neymar alifunga bao lake mwanzoni mwa kipindi cha pili kwa mpira wa adhabu ya moja kwa moja na kumtungua kipa Jung Sung-Ryong kabla ya Oscar kufunga jingine kwa shuti kali.
No comments:
Post a Comment