TFF yatoa vibali kwa nyota wa Tanzania
SHIRIKISHO la Soka Tanzania (TFF) limetoa Hati ya Uhamisho wa Kimataifa (ITC) kwa nyota wawili wa Tanzania kucheza soka chini Afrika Kusini.
Nyota hao ni Robert Kobelo na Mohamed Ibrahim wamepewa hati hizo baada ya kuombewa na Chama cha Mpira wa Miguu Afrika Kusini (SAFA) kama wachezaji wa ridhaa ili wajiunge na klabu ya Cacau United ambayo timu yake inacheza Ligi Daraja la Pili katika Wilaya ya Cacau.
Naye mchezaji Said Maulid aliyejiunga na Ashanti United akitokea nchini Angola msimu huu amepata ITC ambayo sasa inamwezesha kuchezea timu hiyo katika mechi za Ligi Kuu ya Vodacom (VPL) inayoingia mzunguko wake wa tatu kesho.
No comments:
Post a Comment