Nicky Butt amkaribisha Scholes United
Scholes wa mbele kushoto akiwa kwenye benchi la ufundi |
KOCHA wa timu ya vijana Nicky Butt, amemkaribisha Paul Scholes kama kocha msaidizi katika klabu ya Manchester United.
Wachezaji hao maswahiba ambao waliwahi kucheza pamoja katika klabu hiyo.
Butt amemkaribisha Scholes, kwa klabu yake ya vijana kuichapa ile ya Bayer Leverkusen kwa bao 4-3 katika mechi ya kuwania kombe la vijana la UEFA.
Wakati klabu hiyo ikifanya mauaji hayo Scholes(38), alikuwa benchi.
Akimzungumzia mchezaji huyo Butt alisema katika televisheni ya MUTV kuwa "amestaafu soka kwa sasa lakini mtu kama Schole ni muhimu kwa United ambao wameamua kumrejesha katika njia ya kunisaidia.
"Nashukuru kwa Veterani huyu kuja kuungana na klabu hii kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana wa hapa na ninaamini kwa kushirikiana naye tutainua vipaji vingi.
"Ni muhimu kwa ajili yetu kwani atakuwa akionekana katika klabu hii kwa namna anavyokuwa anahitaji."
No comments:
Post a Comment