KOCHA Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kwamba anafurahi kwa kuwa na kikosi imara.
Kutokana na kuwa na kikosi hicho kocha huyo amesema hana mpango wa kusajili mchezaji mwingine yeyote katika usajili wa dirisha dogo la Januari.
Kocha huyo wa Stamford Bridge amesema kuwa anajisifia kuwa na kikosi imara ambacho anaamini kitamvusha vema katika mwaka ujao.
Alisema kuwa "Kikosi chake ni kizuri kwani kimekamilika kila idara na kina wachezaji wadogo hali inayonifanya niamini kwamba Januari hakuna kitakachotukuta na nimezugumza nao na kuwaambia kwamba sihitaji kuona mchezaji akitoka wala kuja hapa.
Alisema "nina mfurahia kila mchezaji na simuhitaji yeyote kujiunga nasi."
Aliongeza kuwa "Sijui kama wao nao wananifurahia, ila kwangu ninafuraha kwa sababu nina wachezaji wengi wazuri na ninafuraha hata wanapofanya vizuri au vibaya, na nimekuwa nikifanya hivyo kwa moyo mweupe." alisema Mourinho
No comments:
Post a Comment