Man United kumzuia Ozil kwenda Arsenal
KLABU ya Manchester United imeungana na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kumsainisha mchezaji wa Ujerumani anayekipiga Real Madrid, Mesut Ozil na leo ikiwa ndio siku ya mwisho wa usajili.
Taarifa hizo zimetolewa na mtandao wa Sky Sports ukisema imekuwa ikitapatapa baada ya kupokea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi iliyopigwa mwishoni mwa wiki hali iliyosababisha kocha David Moyes kupigana kufa na kupona ili kumpata Ozil.
Arsenal, nayo imeonesha nia ya kufanya kufuru katika kuhakikisha inamtwaa mchezaji huyo kwa usajili utakaofikia kiasi cha Euro milioni 42.5.
Kocha wa Arsene Wenger alibainisha mipango yake baada ya kumalizika kwa mechi yao ya jumapili waliyoibuka na ushindi wa kupata bao 1-0 dhidi ya klabu ya Tottenham.
Alisema "tumepanga kufanya maajabu kwa mchezaji huyo katika saa 24 zijazo, ingawa ni uamuzi mgumu lakini wa kushtua." alisema wenger
Ozil (24), alisaini kukipiga Real akitokea Werder Bremen mwaka 2010 kwa dili la euro milioni 15 lakini amekuwa akipambana kutafuta kucheza kikosi cha kwanza.
Ingawa taarifa kutoka Hispania zinasema kuwa mchezaji Ozil hatakwenda kokote bali ataendelea kupigania namba chini ya kocha Carlo Ancelotti.
Kwa nyongeza Ancelotti aliyekuwa akifundisha Paris Saint-Germain anatarajia kuzungumzia suala la Ozil.
No comments:
Post a Comment