Liverpool yapigwa guu la Jini na United
MANCHESTER UNITED walichanua kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Liverpool, bao hilo moja kutoka kwa Javier Hernandez 'CHICHARITO' limeweza kupatia ushindi matajiri wa Jiji la Manchester.
Kwa matokeo hayo, United wamefanikiwa kusonga mbele, ambapo watakutana na Klabu ya Norwich City katika hatua ya nne bora.
Baada ya kushinda mechi hiyo Man Utd itakuwa imepunguza machungu ya kupigwa bao moja kutoka kwa Liverpool kwenye mechi ya Ligi Kuu England wiki chache zilizopita.
Wachezaji wa Arsenal wakishangilia |
Katika mechi nyingine Arsenal wafanikiwa kuwafunga West Brom kwa mbinde kwa mikwaju ya penati 4-3.
Kwa ushindi huo Arsenal watakuta na Chelsea kwenye mzunguko unaofuata.
Hii ni Ratiba ya mzunguko wa nne wa kombe la Ligi
Sunderland v Southampton
Leicester City v Fulham
Birmingham City v Stoke City
Manchester United v Norwich City
Burnley v West Ham United
Arsenal v Chelsea
Tottenham v Hull City
Newcastle v Manchester City
Mechi hizi zitachezwa Jumanne, Oktoba 29 na Jumatano, Oktoba 30
No comments:
Post a Comment