TIMU ya Liverpool jana iliangukia pua katika Ligi Kuu ya England kwa kuchapwa bao 1-0 na Southampton, likifungwa na Dejan Lovren katika dakika ya 53 kwenye Uwanja wa Anfield.
Kichapo hicho kimeifanya Liverpool kubaki na pointi 10 huku Southampton, wakifikisha pointi nane walizovuna kwenye mechi tano walizocheza tangu kuanza kwa msimu huu.
Katika mechi nyingine za ligi hiyo, Chelsea iliibuka na ushindi wa mabao 2 kwa mtungi wakiwafunga Fulham, Newcastle United walifungwa 3-2 na Hull City; West Brimwich walishinda 3-0 dhidi ya Sunderland; West Ham 2, Everton 3 huku Aston Villa wakishinda 1-0 dhidi ya Norwich City.
No comments:
Post a Comment