Lionel Messi ataka taji la Dunia Brazil
MSHAMBULIAJI Lionel Messi amesema baada ya kupata mafanikio makubwa kwa ngazi ya klabu akiwa na Barcelona, kilichobaki ni kung’ara akiwa na Argentina kwa kubeba taji la Dunia mwakani.
Messi, nyota bora mara nne wa dunia, amesema ndoto yake kubwa sasa ni kuiwezesha Argentina kubeba ubingwa wa Kombe la Dunia, mwakani nchini Brazil.
Kauli ya Messi imekuja iku chache tu tangu Argentina chini ya kocha wake Alejandro Sabella, kuvuna ushindi wa mabao 5-2 na kuzidi kuikaribia tiketi ya Brazil.
Kwa ushindi huo wa kishindo katika mechi ya Jumanne wiki hii, Messi
anaamini Argentina yaweza kutwaa ubingwa kama mwaka 1986, ilipofanya hivyo ikiongozwana nyota wake mahiri Diego Maradona kwa wakati huo.
"Naota kutwaa ubingwa wa Kombe la Dunia. Kitu kilichobaki kwangu ni kuisaidia Argentina, japo ni safari ndegu," alisema Messi alipozungumza na waandishi wa habari baada ya kuifunga Paraguay.
"Tumepata tulichokuwa tukitafuta, lakini tulipata wakati mgumu kucheza hapa, lakini tunashukuru kwani kitu muhimu ni kupata tiketi haraka iwezekanavyo.
"Tunataka kuendelea kupata ushindi wa aina hii,” alisema huku akikana habari kwamba Barcelona imetaka asichezea mechi zilizosalia katika kupigania tiketi "Sijui lolote kuhusu hilo, mara zote hupenda kucheza katika kikosi cha Argentina," alisema.
No comments:
Post a Comment