Arsenal yaweka rekodi ya kumsajili Ozil
KLABU ya Arsenal, imefanikiwa kumsajili nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Mesul Ozil kwa kitita cha pauni mil 42.5 kutoka Real Madrid ya Hispania hadi Emirates, mjini London.
Nyota huyo ametua Emirates kwa mkataba wa miaka mitano ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Kocha Arsene Wenger kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mkataba huo, Ozil nyota wa kimataifa wa Ujerumani, mwenye asili ya Uturuki, alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mjini Munich, Ujerumani kabla ya kujiunga rasmi na Arsenal itakayokuwa ikimlipa mshahara wa euro 150,000 na anatarajiwa kuvaa uzi wa Arsenal wenye namba 11.
No comments:
Post a Comment