Usajili wa Kaze wamuweka kazimoto kiporo
WAKATI beki mpya wa wa kimataifa wa Simba Gilbert Kaze
aliyekuwa akicheza
Vital’ O ya Burundi
alitarajiwa kuwasili nchini jana jioni, uongozi wa Simba pamoja unatarajiwa
kukutana na Shirikisho la soka Tanzania (TFF)
kwa ajili ya kumjadili kiungo wake Mwinyi Kazimoto.
Ofisa habari wa Simba Ezekiel Kamwaga alisema jana kwamba,
kama mambo yatakwenda vema Kaze atasaini mkataba wa miaka miwili wa kuichezea
Simba katika michuano mbalimbali itakayoshiriki pamoja na Ligi Kuu Soka
Tanzania Bara.
“Tunashukuru kwamba nafasi ya beki wa Kati ambayo ilikuwa na
mapungufu imepata wahusika hivyo, Kaze sasa ataungana na Mganda Joseph Owino
ambaye pia ni mchezaji mpya tuliyemuongeza kwenye kikosi chetu.
Akizungumzia suala la Kazimoto, Kamwaga alikiri kwamba
wamepokea ofa kutoka timu ya moja ya Qatar lakini ni ofa ndogo sana ambayo
hawawezi kuikubali kwani thamani yake haifikii ile waliyomuhamishia kutoka JKT
Ruvu.
Hata hivyo, Kamwaga alisema hawezi kuzungumzia kwa undani
juu ya suala la Kazimoto kutokana na ukweli kwamba bado ana maswali ya kujibu
Watanzania na klabu yake ya Simba kwa ujumla.
“Suala la Kazimoto tumeliweka pembeni kwani tunatarajia
kukaa na TFF kwa ajili ya kumjadili na baada ya hapo mambo mengine kuhusu yeye
yatafuata,”alisema
Ikumbukwe kuwa, Kazimoto alitimkia Qatar hivi karibuni baada
ya kutoroka katika kambi ya timu ya Taifa siku ambayo ilikwaanza na Uganda ‘The
Cranes’ katika mchezo wa kuwania kufuzu fainali za Afrika zinazoshirikisha
wachezaji wanaocheza ligi za ndani (CHAN).
Kazimoto aliyesajiliwa na Simba kutoka JKT Ruvu alikwenda
kujaribiwa na klabu ya Al Markhiya Sc inayoshiriki Ligi daraja la kwanza ya
huko na kufuzu na hivyo wakala wake, Mahmoud Abu Al Ght kuwasiliana na uongozi
wa Simba kwa ajili ya ofa hiyo.
Katika hatua nyingine, kiungo Mganda anayewaniwa na Simba
Moses Oloya amekana kusaini mkataba wa kujiunga na mahasimu wao wa jadi, Yanga.
Kamwaga alisema kwamba Oloya amezungumza kwa simu na
Mwenyekiti wa Simba Alhaj Ismail Aden Rage akisema anashangazwa na taaarifa
hizo kwani kwa sasa anafanya mazungumzo na uongozi wa Simba na mambo yakienda
vizuri atasaini mkataba.
“Oloya amewataka wanachama wa Simba kutulia kwani anafafanya
mazungumzo na uongozi wa Simba tu na akili yake ni kuichezea Simba iwapo
mazungumzo hayo yatafikia muafaka,”alisema Kamwaga.
No comments:
Post a Comment