Serikali yakiri dosari Katiba TFF
Rais wa TFF, Leodegar Tenga |
Kauli hiyo imekuja ikiwa ni siku moja tu tangu Gazeti Tanzania Daima liandike habari ya katiba hiyo kukwama kwa msajili kutokana na marekebisho
kupitishwa pasipo kupigiwa kura kama ibara ya 30 (iii) inavyotaka pamoja.
Dosari nyingine ambayo ilielezwa awali iliyomfanya Msajili
Mercy Rwezaura kusita kupisha marekebisho hayo, ni kitendo cha TFF kuunfa
Kamati za Maadili kabla ya katiba hiyo kupata baraka rasmi za ofisi yake.
Akizungumza na Chanzo chetu cha habari kwa njia ya simu kutokea
Jimboni kwake Mvomero, Morogoro, Naibu Waziri Amos Makala, alikiri kuarifiwa
jambo hilo na Msajili kuwa mchakato wa
upitishaji marekebisho hayo una dosari kwa mujibu wa katiba.
“Ni kweli nimejulisha na ofisi ya Msajili kuwa kuna dosari,
tena tunataka TFF wenyewe wawaeleze ukweli Watanzania kwa sababu wakati mwingi serikali imekjuwa
ikitupiwa lawama kwamba inataka kuharibu mambo,” alisema Makala.
Akifafanua zaidi, Makala alihoji inawezekana vipi
marekebisho ya uundwaji wa Kamati za Maaadili kabla ya kupata baraka za Ofisi
ya Msajili, wao TFF tayari wameshaunda Kamati husika na kutangaza wajumbe wake.
“Hivi inaingia akilini kweli, ninyi mmefanya mabadiliko ya
katiba ili itambue uwezpo wa Kamati za Maadili na mmepeleka kwa Msajili ipate
baraka, lakini kabla haijapita, ninyi mnaziunda kamati,” alihoji Makala.
Alipoulizwa juu ya hatma ya uchaguzi mkuu wa Shirikisho hilo
ambao umetakiwa uwe umefanyika hadi kufikia Oktoba 30 mwaka huu, Waziri Makala
alisema lolote litakalotokea mbelke ya safari, Serikali haipaswi kulaumiwa.
“Kuhusu ukomo wa muda ambao Fifa (Shirikisho la soka la
Kimataifa) limetaka kwa kipindi fulani uchaguzi mkuu uwe umefanyika, sisi hilo
tunawaachia TFF wenyewe waamue nini cha kufanya, sisi tunaangalia sheria na
taratibu za nchi zinasema nini,” alisema.
Utata huo katika marekebisho ya Katiba yaliyofanywa kwa
maelekezo ya Fifa, ni mwendelezo wa mchakato wa uchaguzi wa shirikisho hilo
kuwa na dosari kwani
awali ulipangwa kufanyika Februari 24, lakini ukasimamishwa.
Hata hivyo, wataalamu wa masuala ya soka, wanasema pamoja na
mapungufu hayo, katiba hiyo inaweza
kupitishwa na Msajili, lakini kabla haijatumika kwenye uchaguzi, itapaswa
kupata baraka za Mkutano Mkuu kisha kugongwa mhuri siku hiyo.
No comments:
Post a Comment