JAPO Kocha wa Manchester United, David Moyes amekuwa akisema Wayne Rooney hatoki Old Trafford, viongozi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na Chelsea.
Yaelezwa mpango huo unakwenda pamoja na Juan Mata kwenda Old Trafford kama Rooney atakwenda Stamford Bridge.
Nje ya Mata, mazungumzo yamejikita kwenye thamani ya Rooney kutokana na United kutaka pauni mil 40 huku Chelsea ikiwa tayari kwa pauni mil 28.
Mpango huo unafanyika wakati ambapo Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akisema bado anahitaji mshambuliaji, iwe kutoka Old Trafford au kwingineko.
No comments:
Post a Comment