KLABU ya Borussia Dortmund imeamua kumaliza mvutano kati yake na mshambuliaji kimataifa wa Poland, Robert Lewandowski, aliyekuwa akitaka kuhama kwa kutoridhishwa na mshahara wake.
Kwa mujibu wa habari zilizopatikana na kuthibitishwa na uongozi wa klabu hiyo, nyota huyo aliyetoa mchango mkubwa kwa timu hiyo kufika fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya, atalipwa mara tatu ya mshahara aliokuwa akilipwa.
Baada ya fainali ya Ligi ya Mabingwa iliyochezwa Mei 25 kwenye Uwanja wa Wembley, mjini London ambayo walifungwa na Bayern Munich, Lewandowski akawa lulu lakini akiwekewa ngumu kuhama.
Klabu yake iligoma kumruhusu kwa hoja kuwa ingefanya hivyo mwakani, hivyo nyota huyo kuamua kubaki kwa shingo upande.
Kuhusu maslahi, jarida la michezo la Bild, limedokeza kuwa klabu hiyo imemalizana na nyota huyo kwa kuyafanyia kazi madai yake yote ambayo awali yalikuwa vigumu kutekelezwa.
Licha ya klabu hiyo kukiri kufanyia kazi madai ya mchezaji huyo, ikiwemo kumwongezea mshahara, haijaweza wazi ni kwa kiwango gani.
Hata hivyo, kuna habari kuwa nyota huyo sasa atakuwa akilipwa mshahara wa euro mil 5, badala ya ule wa awali wa euro mil 1.5 kwa mwaka.
No comments:
Post a Comment