Eto'o njiani kukamilisha usajili Chelsea
CHELSEA inatarajia kumsajili Samuel Eto’o kwa dau la euro
milioni 7 kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kukiri kushindwa kumtwaa
mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 32 kutoka Cameroon,
anatarajiwa kulamba mshahara wa Euro milioni 17 kwa mwaka hali itakayomfanya
kuwa mchezaji anayelipwa zaidi akiwa anatokea katika klabu ya Russia ya Anzhi
Makhachkala.
Ingawa klabu yake ya Anzhi imeonesha nia ya kutaka
kumuongezea muda na imemuahidi kumuongezea mshahara maradufu wa huo anaoahidiwa
na Chelsea.
Eto'o alifika London, kituo cha St Pancras siku ya jumatano
usiku, ikiwa ni pamoja na kupima vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na
Chelsea.
Willian akiwa kwenye Uzi mpya wa Chelsea |
Kwa kumtaka mshambuliaji huyo Mourinho anaonekana kama
anacheza kamari na wale wanaommezea mate Eto’o.
Uwezekano wa kuchukuliwa Etoo ni mkubwa kutokana na mwenyewe
kuonesha nia ya kuwa chini ya kocha Mourinho ambaye anamwagia sifa kwa kusema “nimepita
kwa makocha wengi wazuri lakini kwa Jose hakuna anayefanana naye,” alisema Eto’o
No comments:
Post a Comment