Masikini Taifa Stars Yakosa
tiketi ya CHAN mwaka 2014
Kiungo Mtanzania, Amir Kiemba alipambana ndani ya Uwanja wa Taifa wa Mandela. (Picha kwa hisani ya IssaMichuzi BLOG) |
Ndivyo ilivyo kwa timu
hiyo ambayo baada ya Juni 8 kupoteza nafasi ya kucheza fainali za Kombe la
Dunia nchini Brazil, jana imeshindwa tena kupata tikjeti ya fainali za Afrika
kwa nyota wa Ligi za Ndani-CHAN.
Kwa kipigo cha siku hiyo
cha mabao 4-2 kutoka kwa Ivory Coast
kwenye Uwanja wa Taifa jijini Dar es
Salaam , kikafuta hesabu za
Brazil, hivyo turufu pekee
ilikuwa ni fainali za CHAN nchini Afrika Kusini, pia za mwakani.
Katika mechi ya jana
iliyochezwa kwenye Uwanja wa Taifa wa Mandela, mjini Namboole, nje kidogo ya
Kampala, Stars wakiwa nyuma kwa bao 1-0 walilofungwa Julai 13, jijini Dar es Salaam , walifungwa
tena 3-1.
Kwa idadi mabao 4-1, sio
tu imeitupa Stars nje ya vita hiyo ya kwenda Brazil
na kuipa Uganda
tiketi ya Afrika Kusini, pia imetoa jawabu kwamba kazi kubwa inahitajika ili
kuwa na timu bora.
Stars iliyocheza fainali
za kwanza nchini Ivory Coast mwaka 2009 chini ya Mbrazil Marcio Maximo, ilimaliza
kipindi cha kwanza kwa sare ya bao 1-1.
Wenyeji walioanza kufunga
bao dakika ya saba katika mechi iliyochezeshwa na Kanoso Abdoul Ohabee kutoka
Madagascar, likifungwa na Frank Kalanda akimalizia mpira uliopigwa ndani ya eneo la hatari la Stars.
Bao hilo liliwafanya Stars
watulie zaidi na kufanikiwa kusawazisha dakika ya 18, mfungaji akiwa Amri
Kiemba kutokana na pasi nzuri ya Mrisho Ngasa kwenye
kona ya eneo la mita 18.
Dakika ya 32 nusura Stars
ipate bao, lakini mkwaju maridadi wa Ngasa ambao tayari ulikuwa umempira kipa Hamza
Muwonge, uligonga mwamba kabla ya kuokolewa na mabeki.
Mabao la pili la wenyeji
katika mechi hiyo lilifungwa dakika ya 48, Brian Majwega kabla ya Kalanda
kuongeza la tatu dakika ya 63, kutokana na makosa ya Salum Abubakar kupokwa mpira
akiwa kwenye nafasi nzuri ya kutoa pasi kwa mwenzake.
Kocha Kim Poulsen alifanya
mabadiliko dakika ya 43, akimwingiza Simon Msuva badala ya Frank Domayo
aliyeumia na dakika ya 78 akawaingiza kwa mpigo Haruna Chanongo na Vincent
Barnabas na kuwatoa David Luhende na John Bocco.
Hata hivyo mabadiliko hayo
hayakubadili matokeo ya mchezo ambapo hadi mwisho, wenyeji Uganda waliibuka na suhindi wa
mabao 3-1, hivyo kujitwalia tiketi ya Afrika Kusini kwa jumnla ya mabao 4-1.
Kikosi cha Stars
kilipangwa hivi; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, David Luhende/Vincent Barnabas,
Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Athuman Idd, Frank Domayo/Simon Msuva, Salum
Abubakar, John Bocco/Haruni Chanongo, Amri Kiemba na Mrisho Ngasa.
Stars inayodhaminiwa na
Kilimanjaro Premium Lager itarejea nyumbani leo saa 4 usiku kwa ndege ya
PrecisionAir.
No comments:
Post a Comment