Man City wampa kiwewe Mourinho
Jose Mourinho |
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema Manchester City
watakuwa washindani wakubwa katika Ligi Kuu
hasa baada ya kufanya usajili wa nguvu chini ya kocha mpya,
Manuel Pellegrini.
Kauli ya Mourinho, inatokana na Man City kutumia gharama
kubwa kuwasajili nyota kadhaa kama Alvaro Negredo, Stevan Jovetic na Jesus
Navas.
Pamoja na usajili huo, Mourinho anaamini Manchester City
walipaswa kufanya kwanza tathmini ya
usajili wa msimu uliopita.
City imetumia kiasi cha pauni mil 100 kupata saini ya
Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk, Jesus Navas na Alvaro Negredo kutoka
Sevilla na Stevan Jovetic kutoka Montenegro.
Mourinho aliyerejea Chelsea akitokea Real Madrid, amesema
kwa usajili huo, Man City watakuwa washindani wakubwa msimu ujao.
Alipoulizwa juu ya kumwania Wayne Rooney, alisema hawezi kusema lolote.
Alipoulizwa juu ya kumwania Wayne Rooney, alisema hawezi kusema lolote.
No comments:
Post a Comment