Wednesday, November 6, 2013

Klopp aipiga vijembe Arsenal

Jurgen Klopp aipiga vijembe Arsenal
Makocha Wenger (kushoto), na Klopp.


KOCHA wa Borussia Dortmund ya Ujerumani, Jurgen Klopp ameiponda Arsenal kwa kuifananisha na muziki mkubwa usio na sauti kuelekea mechi ya leo usiku ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

Klopp alisema kuwa pamoja na timu hiyo kucheza soka ya kuvutia kwa namna ya kupiga chenga, kumiliki na kupiga pasi nyingi, lakini ni kama kuziki usio na sauti.
"Kwangu, 'Sir' Arsene Wenger, nampenda sana," alisema Klopp ambaye katika mechi iliyopita vijana wake walishinda 2-1 na kuongeza:
“Arsenal imekuwa imara kwa miaka 10. Lakini ni kama muziki usio na sauti tofauti na wao ambao ni soka yetu kwani ni kama chuma kizito chenye kishindo.

No comments:

Post a Comment