Chelsea yaitungua Norwich City,
TIMU ya Chelsea, jana ilivuna ushindi wa ugenini wa mabao 3-1 dhidi ya Norwich City, ikiwa ni faraja nyingine kwa Kocha Jose Mourinho shukrani kwa Oscar aliyetangulia kufunga dakika ya tatu kwenye Uwanja wa Carrow Road.
Bao la pili la Chelsea, lilifungwa na mtokea benchi, Eden Hazard kabla ya Willian kufunga la tatu, hivyo wakali hao wa Stamford Bridge kuondoka na ushindi huo mnono.
Norwich City walipata bao hilo moja mwanzoni mwa kipindi cha pili likifungwa na Anthony Pilkington. Ushindi huo umeiwezesha Chelsea kufikisha pointi 13.
Kwa upande mwingine Timu ya Arsenal ilitoka sare ya mabao 1-1 dhidi ya West Brom, ambapo wenyeji walitangulia kupata bao moja kupitia mchezaji wao Claudio Yacob kipindi cha kwanza.
Jack Wilshere ndiye aliyeisawazishia Arsenal dakika ya 63, mpaka filimbi ya mwisho inapulizwa hakuna timu iliyoibuka kifua mbele.
No comments:
Post a Comment