Saturday, September 14, 2013

Man United, Arsenal moto chini England

Man United, Arsenal moto chini England
TIMU ya Arsenal imevuna pointi tatu baada ya kuifunga Sunderland mabao 3-1 kwenye dimba la Stadium of Light huku Manchester United ikiifunga Crystal Palace 2-1 kwenye Uwanja wa Old Trafford.
Kwa ushindi huo Arsenal imefikisha pointi tisa kama Tottenham na Liverpool ambayo kesho usiku itacheza na Swansea.
Man United ilipata ushindi wa kwanza kwenye Uwanja wake kwa msimu huu kwa bao la penalti ya kipindi cha kwanza kupitia kwa Robin van Persie kabla ya Wayne Rooney kufunga la pili na kufikisha pointi saba.

No comments:

Post a Comment