Wamiliki wakana kuiuza Liverpool
KAMPUNI ya Fenway Sports Group (FSG) imezikana
taarifa za vyombo vya habari zilizodai kuwa inajiandaa kuiuza klabu ya Liverpool .
Magazeti yaliripoti Ijumaa, mabilionea wawili
raia wa Marekani na kampuni moja ya Saudia inayojihusisha na uuzaji wa mafuta,
zimeingia katika mazungumzo ya kuinunua Liverpool
kutoka kwa FSG, ambayo ilidaiwa kutaka dau la pauni milioni 350.
Kutokana na taarifa hizo, kwa pamoja FSG na
Liverpool zimekanusha kwa nguvu moja habari hizo na wamiliki wa Kimarekani
ambao walianza kuimiliki Liverpool tangu Oktoba 2010, walielezea nia yao ya kuendelea kubaki
Anfield.
Msemaji wa Fenway Sports Group alisema: “Kama ulivyowahi kuwa uvumi mwingine wowote kuhusu kuuzwa
kwa Liverpool Football Club, hakuna ukweli wowote pia katika tetesi hizi.
“Hatujawahi kuwa na mkutano na mtu yeyote kuhusu
kuiuza klabu, hatujui ni nani hasa chanzo cha uvumi huo, na lolote
linalohusiana na upotoshaji juu ya mauzo ya Liverpool .”
Naye msemaji wa Liverpool ,
akaongeza: “Fenway Sports Group imeweka wazi kila kitu Liverpool Football
Club haiuzwi. Hakuna ukweli wowote katika habari hiyo.”
No comments:
Post a Comment