CASTLE LAGER yaileta Barcelona Afrika
BIA ya Castle Lager, jana
iliingia makubaliano ya kuidhamini klabu maarufu Duniani, FC Barcelona ya
Hispania kwa kipindi cha miaka mitatu udhamini
utakaokifanya kinywaji
hicho kuwa bia rasmi ya klabu
hiyo Afrika.
Hafla ya ushirikiano huo
iliyofanyika kwenye uwanja wa Camp Nou , unaifanya CASTLE Lager kuwa bia rasmi
itakayotumika kwa shughuli yoyote ambayo Barcelona
itashiriki Afrika.
Aidha, chini ya ushirikiano
huo, FC Barcelona itafungua milango kwa
mashabiki wake Barcelona Afrika kuwa karibu na wachezaji wa Barcelona , vifaa na kumbukumbu.
Aidha, itapata nafasi ya
kusafiri kwenda Hispania kushuhudia kwa karibu timu ya Barcelona .
Mkataba huu utakuwa maalum
kwa ajili ya CASTLE Lager kwenye nchi nyingi za Afrika isipokuwa kwa baadhi ya
nchi chache zilizochaguliwa ambapo itatumika Castle Milk Stout.
Ni mara ya kwanza kwa timu ya
FC Barcelona kusaini mkataba
wa udhamini na kampuni ya
bara la Afrika. Kushirikiana na bia bingwa Afrika litaongeza kwa haraka
umaarufu wa timu ya FC Barcelona ndani ya bara la Afrika na kufungua milango
kwa mashabiki wa klabu hii kupata bidhaa mbalimbali za Barcelona na nafasi za
kushinda safari ya kwenda Barcelona kuitembelea klabu hiyo.
“Tumefurahi sana kuingia katika ushirikiano na Castle
Lager na Castle Milk Stout, chapa zinayofahamika dunia nzima. Tunafanana na
Castle kwa kuwa sote tuna historia ya zaidi ya miaka 100 na utamaduni
uliotukuka. Na sote tuna mapenzi na mpira wa miguu pamoja na mashabiki wake katika
soko muhimu kama Afrika,” alisema Javier Faus,
Makamu wa Rais wa FC Barcelona anayeshughulikia masuala ya uchumi.
“Uamuzi wa Barcelona kuingia
ushirika na na bia inayoongoza barani Afrika kutaongeza umaarufu wa bia hiyo
kwenye bara hili na kuwawezesha wachezaji wa timu hiyo kufika maeneo amabyo
hawajawahi kufika barani Afrika,” alisema David
Carruthers Mkurugenzi wa Masoko wa SabMiller Afrika (kampuni mama ya
TBL).
CASTLE Lager si bidhaa mpya
kwenye udhamini wa mpira wa miguu na vyama, ina miaka mingi ya kujihusisha
katika soka barani Afrika kwa kipindi cha miaka 85 kupitia ligi mbalimbali za
nchi tofauti kama vile Zimbabwe ,
Swaziland , Botswana , Lesotho
na pia mashindano ya kanda kama COSAFA Kusini
mwa Afrika na CECAFA Afrika Mashariki.
Kutokana na soka la Ulaya
kupata umaarufu mkubwa na mashabiki wengi barani Afrika, Castle Lager imekuwa
ikidhamini urushaji wa matangazo ya ligi hizo kwenye televisheni barani
Afrikana kuwapa mashabiki fursa ya kufatilia kila kinachoendelea kwenye ligi
hizo maarufu duniani ambazo ni Ligi Kuu ya Ulaya, Ligi Kuu ya Uingereza na La
Liga ya Kihispania.
Kufuatia udhamini huu,
wanywaji wa Castle Lager na Castle Milk Stout pamoja na mashabiki wa Barcelona barani Afrika
sasa watarajie mambo mengi ya kusisimua katika ulimwengu wa soka.
No comments:
Post a Comment