Simba wamvutia kasi Oloya
Moses Oloya |
KLABU
ya Simba inamsubiri kiungo wa kimataifa wa Uganda, Moses Oloya avunje mkataba
na Saigon Xuan Than ya Vetinam ili impatie mkataba wa kuitumikia kwa msimu
ujao.
Hiyo
inakuja siku chache baada ya kuwatimua nyota wanne wa kigeni kutokana na
kutorishishwa na viwango vyao ambao ni Mussa Mudde, Assumani Buyinza, Samuel
Ssenkoomi, Felix Cuipo na James Kun.
Kutemwa
kwa nyota hao, kunaifanya Simba kusaliwa na wageni wawili ambao ni kipa Abel
Dhaira na mshambuliaji mpya Amissi Tambwe, raia wa Burundi anayetarajiwa Siku
ya Simba (Simba Day) itakayofanyika mwezi ujao.
Kwa
mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Usajili ya klabu hiyo, Zacharia Hans Pope, wiki
iliyopita alizungumza na Oloya na kuahidi atakuja nchini baada ya kuvunja
mkataba wake
na
Saigon.
“Ijumaa
wiki iliyopita, nilizungumza naye (Oloya), akaniambia yuko katika hatua za
mwisho kuvunja mkataba wake, baada ya kufanikiwa hilo atakuja kusaini rasmi Simba,”
alisema na kuongeza kuwa msimu huu wameamua kufanya usajili kwa utulivu mkubwa.
Pope
alisema kama watafanikiwa kupata saini kiungo huyo, wanaimani msimu ujao watakuwa
na kikosi imara hivyo kufanya vizuri kwenye Ligi Kuu kutokana na uwezo wa
mchezaji huyo.
Alisema
hata kama itatokea wakamkosa nyota huyo kwa ajili ya raundi ya kwanza ya ligi
hiyo itakayoanza Agosti 24, watahakikisha wanafanikisha wanakuwa naye katika
raundi ya pili kutokana na mchezaji huyo kukubali kutua Msimbazi.
Oloya, kiungo alitezaliwa Oktoba 22, mwaka 1992, kabla ya kutimkia Vietnam, msimu wa 2009/10 aliichezea KCC ya Uganda kabla ya kutua Saigon mwaka 2011 na kuichezea mechi 29 hadi sasa, akifunga mabao matano. Ameichezea Uganda mechi 22.
Oloya, kiungo alitezaliwa Oktoba 22, mwaka 1992, kabla ya kutimkia Vietnam, msimu wa 2009/10 aliichezea KCC ya Uganda kabla ya kutua Saigon mwaka 2011 na kuichezea mechi 29 hadi sasa, akifunga mabao matano. Ameichezea Uganda mechi 22.
No comments:
Post a Comment