Kiiza kubanwa Jangwani
WAKATI nyota wake wa kimataifa, Mganda Hamis Kiiza,
alitarajiwa kuwasili jana, uongozi wa Yanga umepanga kumbana awapatie barua ya
klabu aliyokwenda kufanya majaribio nchini Serbia kabla ya kumatia mkataba
mpya.
Usajili wa Kiiza umegubikwa na utata kutokana na nyota huyo kuhitaji dau la sh mil. 45 huku uongozi
ukitaka kumpa sh mil. 35 kwa mafungu, jambo ambalo linapingwa na nyota huyo.
Habari kutoka katika klabu hiyo zimedokeza kama mchezaji
huyo atarejea na barua anaweza kusaini mkataba mpya wa Mil. 35 na kwamba si zaidi
ya kiasi hicho.
Chanzo hicho kiliongeza kuwa Kiiza amekuwa akiwachanganya
vichwa kwani amekuwa akihitaji mshahara si chini ya dola 1,000 na dola 2,000 za
usajili kwa kila mwezi.
No comments:
Post a Comment