Kazimoto afaulu majaribio Qatar
KLABU ya Al Markhiya Sports Club ya Doha, Qatar imetuma
barua kwa uongozi wa Simba ukiomba umruhusu kiungo wake Mwinyi Kazimoto
kujiunga na timu hiyo baada ya nyota kufanya vizuri katika majaribia yake hivi
karibuni.
Habari za uhakika zinasema, Kazimoto aliyekwenda Qatar wiki
iliyopita kusaka nafasi ya kucheza soka la kulipwa katika klabu hiyo,
ameshafanyiwa vipimo vyote hivyo kinachotakiwa ni kibali tu kwa ajili ya
kuichezea timu hiyo iliyoasisiwa mwaka 1995 ambayo sasa inacheza Ligi Daraja la
Pili.
Japo nyota huyo aliondoka bila idhini ya viongozi wa Simba
wala wa Shirikisho la soka Tanzania (TFF) kutokana na kuondoka nchini akitokea
kambi ya timu ya soka ya Tanzania, Taifa Stars,
Al Markhiya imeiangukia Simba kuomba ridhaa yake.
Tanzania Daima ilipoutafuta uongozi wa Simba kuhusu jambo
hilo, kiongozi mmoja wa Simba alikiri kuwepo kwa barua hiyo iliyoandikwa na
Mohamed Abu Ali, lakini wenye mamlaka juu ya uamuzi huo ni viongozi wa juu wa
klabu.
“Kweli kuna hiyo kitu, lakini siwezi kulizungumzia kwa
undani zaidi kwani sina uamuzi juu ya hili na hasa ikizingatiwa mazingira
ambayo mchezaji mwenyewe aliondoka sasa tuwaachie viongozi wenye
mamlaka,”alisema
Hata hivyo hakuna kiongozi yoyote wa juu wa Simba aliyeweza kupatika jana baada ya
kutopokea simu zao za viganjani.
Kama Kazimoto atapata baraka kutoka kwa uongozi wa Simba
atakuwa ni miongoni mwa nyota wa Tanzania wanaopata ulaji wa kutakata kupitia
soka la kulipwa.
No comments:
Post a Comment