BAYERN wamepata pigo baada ya kiungo wake wa kimataifa wa Hispania, Thiago Alcantara kuumia misuli ya katika kifundo cha mguu, hivyo atalazimika kuwa nje ya dimba kwa wiki saba.
Majeraha hayo aliyapata juzi wakati Timu yake ya Bayern ikishinda mabao 2-0 dhidi ya Nurnberg katika mechi ya Bundesliga iliyochezwa kwenye Uwanja wa Allianz Arena, mjini Munich.
Katika mechi hiyo, Franck Ribery alifunga bao la kwanza katika dakika ya 69 kabla ya Arjen Robben kufunga jingine huku David Alaba akikosa penalti katika dakika za awali katika mechi hiyo.
Kwa ushindi huo, Bayern sasa wamefikisha pointi tisa, baada ya kushinda mechi zote tatu tangu kuanza kwa msimu.

No comments:
Post a Comment