Robben awatuliza wenzake Bayern
MCHEZAJI mahiri wa Bayern Munich, Arjen Robben, amewaambia
wachezaji wanzake hawana sababu ya
‘kupaniki’ kwa kufungwa mabao 4-2 na wapinzani wao, Borussia
Dortmund, katika mechi ya Supercup.
Kipigo hicho cha mwishoni mwa wiki kwa kiasi kikubwa
kimewachanganya Bayern wakizingatia ni mechi ya ufunguzi wa Bundesliga, tena
wakiwa chini ya Kocha mpya, Pep Guardiola.
Zaidi ya hilo, kipigo hicho ni kama kuwadhalilisha wakali
hao waliomaliza msimu uliopita wakiwa na mataji matatu, Bundesliga, Ligi ya Mabingwa Ulaya na Kombe
la Ujerumani.
Aidha, kipigo katika mechi hiyo ya kuukaribisha msimu mpya
wa Bundesliga, kumemzuia Kocha mpya, Pep Guardiola kuonja radha ya ubingwa
kabla ya kuanza kwa Bundesliga.
Katika mechi hiyo, Borussia chini ya Kocha wake, Jurgen
Klopp, walionesha soka ya nguvu kiasi cha kuwafunika mabingwa hao wa Ulaya,
matokeo ambayo yameonekana kuwavunja moyo baadhi yao.
“Hatuna sababu ya ‘kupaniki’, tuangalie kiwango chetu, kwa
upande wangu sina hofu kabisa,” alisema Robben alipozungumza na mtandao wa TZ
huku akiwapongeza Borussia kwa kucheza vizuri.
“Nawapongeza Dortmund. Walistahili kushinda. Lakini kufungwa
kwetu hakuna maana kuwa tumecheza hovyo.
“Sidhani kama mabao manne yametokana na staili yetu ya
kushambulia katika mechi ile, hatupaswi kupoteza muda kufikiria kipigo, tujifunze
kutokana na makosa.
Mabingwa Bayern wataanza kampeni ya kutetea taji la Bundesliga Agosti 10 kwa kuwakaribisha Greuther Furth.
Mabingwa Bayern wataanza kampeni ya kutetea taji la Bundesliga Agosti 10 kwa kuwakaribisha Greuther Furth.
No comments:
Post a Comment