Thursday, August 29, 2013

Eto'o njiani kukamilisha usajili Chelsea

Eto'o njiani kukamilisha usajili Chelsea
CHELSEA inatarajia kumsajili Samuel Eto’o kwa dau la euro milioni 7 kwa mkataba wa mwaka mmoja baada ya kukiri kushindwa kumtwaa mshambuliaji wa Manchester United, Wayne Rooney.
Mshambuliaji huyo mwenye miaka 32 kutoka Cameroon, anatarajiwa kulamba mshahara wa Euro milioni 17 kwa mwaka hali itakayomfanya kuwa mchezaji anayelipwa zaidi akiwa anatokea katika klabu ya Russia ya Anzhi Makhachkala.
Ingawa klabu yake ya Anzhi imeonesha nia ya kutaka kumuongezea muda na imemuahidi kumuongezea mshahara maradufu wa huo anaoahidiwa na Chelsea.
Eto'o alifika London, kituo cha St Pancras siku ya jumatano usiku, ikiwa ni pamoja na kupima vipimo vya afya kwa ajili ya kujiunga na Chelsea.
Willian akiwa kwenye Uzi mpya wa Chelsea
Klabu yake hiyo imekuwa na uhusiano mzuri na Chelsea kwani imeshawapatia mchezaji wao mwingine wa Brazili anayekwenda kwa jina la Willian.
Kwa kumtaka mshambuliaji huyo Mourinho anaonekana kama anacheza kamari na wale wanaommezea mate Eto’o.
Uwezekano wa kuchukuliwa Etoo ni mkubwa kutokana na mwenyewe kuonesha nia ya kuwa chini ya kocha Mourinho ambaye anamwagia sifa kwa kusema “nimepita kwa makocha wengi wazuri lakini kwa Jose hakuna anayefanana naye,” alisema Eto’o

No comments:

Post a Comment