Monday, September 2, 2013

Henry Joseph aitwa tena Taifa Stars

Henry Joseph aitwa tena Taifa Stars
KOCHA Mkuu wa Taifa Stars, Kim Poulsen amemjumuisha mchezaji Henry Joseph wa Simba kwenye kikosi chake kinachojiandaa kwa mechi ya mchujo ya Kombe la Dunia dhidi ya Gambia itakayochezwa Septemba 7 mwaka huu jijini Banjul.
Tayari Joseph amesharipoti kwenye kambi ya timu hiyo iliyoko hoteli ya Accomondia jijini Dar es Salaam. Taifa Stars imeingia kambini tangu Agosti 29 mwaka huu, itafanya mazoezi yake kwenye Uwanja wa Kumbukumbu ya Karume.
Programu ya timu hiyo inaonesha kuwa kesho itafanya mazoezi yake asubuhi na jioni kwenye uwanja huo huo wa Kumbukumbu ya Karume.
Wakati huo huo, kesho saa 6 kamili mchana Kocha Kim Poulsen atakuwa na Mkutano na Waandishi wa Habari.

Arsenal yaweka rekodi ya kumsajili Ozil

Arsenal yaweka rekodi ya kumsajili Ozil

KLABU ya Arsenal, imefanikiwa kumsajili nyota wa kimataifa wa Ujerumani, Mesul Ozil kwa kitita cha pauni mil 42.5  kutoka Real Madrid ya Hispania hadi Emirates, mjini London.
Nyota huyo ametua Emirates kwa mkataba wa miaka mitano ikiwa ni sehemu ya mikakati ya Kocha Arsene Wenger kuimarisha kikosi chake kwa ajili ya Ligi Kuu ya England na Ligi ya Mabingwa Ulaya.
Kwa mkataba huo, Ozil nyota wa kimataifa wa Ujerumani, mwenye asili ya Uturuki, alitarajiwa kufanyiwa vipimo vya afya mjini Munich, Ujerumani kabla ya kujiunga rasmi na Arsenal itakayokuwa ikimlipa mshahara wa euro 150,000 na anatarajiwa kuvaa uzi wa Arsenal wenye namba 11.

Kaka arejea nyumbani AC Milan

Kaka arejea nyumbani AC Milan
MAKAMU wa rais wa klabu ya AC Milan, Adriano Galliani amethibitisha klabu yake kumsainisha mchezaji Ricardo Kaka anayekipiga Real Madrid.
Kaka anatarajiwa kurejea Milan, ambako anaamini atafurahia maisha yake ya soka, baada ya kukaa Bernabeu kwa muda wa miaka minne kwa dili la pauni milioni 56.
Mchezaji huyo mwenye miaka 31 amekubali kusaini mkataba wa miaka miwili mwishoni mwa wiki hii.
Kaka alikosa raha katika muda wake wa uchezaji kutokana na kusombuliwa na majeruhi.
Lakini mchezaji huyo wa kimataifa wa Brazil anaamini kiwango chake kitarudi kama zamani mara ya kwanza alipokuwa San Siro.
Taarifa za Milan zimeeleza kuwa: "usiku wa jana tumeboresha zaidi uhusiano wetu na klabu za Real Madrid kwa kuwezesha kuturudishia mchezaji Ricardo Kaka.

Man United kumzuia Ozil kwenda Arsenal

Man United kumzuia Ozil kwenda Arsenal 
KLABU ya Manchester United imeungana na Arsenal katika kinyang’anyiro cha kumsainisha mchezaji wa Ujerumani anayekipiga Real Madrid, Mesut Ozil na leo ikiwa ndio siku ya mwisho wa usajili.
Taarifa hizo zimetolewa na mtandao wa Sky Sports ukisema imekuwa ikitapatapa baada ya kupokea kipigo cha 1-0 dhidi ya Liverpool katika mechi iliyopigwa mwishoni mwa wiki hali iliyosababisha kocha David Moyes kupigana kufa na kupona ili kumpata Ozil.
Arsenal, nayo imeonesha nia ya kufanya kufuru katika kuhakikisha inamtwaa mchezaji huyo kwa usajili utakaofikia kiasi cha Euro milioni 42.5.
Kocha wa Arsene Wenger alibainisha mipango yake baada ya kumalizika kwa mechi yao ya jumapili waliyoibuka na ushindi wa kupata bao 1-0 dhidi ya klabu ya Tottenham.
Alisema "tumepanga kufanya maajabu kwa mchezaji huyo katika saa 24 zijazo, ingawa ni uamuzi mgumu lakini wa kushtua." alisema wenger
Ozil (24), alisaini kukipiga Real akitokea Werder Bremen mwaka 2010 kwa dili la euro milioni 15 lakini amekuwa akipambana kutafuta kucheza kikosi cha kwanza.
Ingawa taarifa kutoka Hispania zinasema kuwa mchezaji Ozil hatakwenda kokote bali ataendelea kupigania namba chini ya kocha Carlo Ancelotti.
Kwa nyongeza Ancelotti aliyekuwa akifundisha Paris Saint-Germain anatarajia kuzungumzia suala la Ozil.

Gareth Bale ni Mchezaji rasmi wa Madrid

Gareth Bale ni Mchezaji rasmi wa Madrid

Bale alipokuwa akipima afya kwenye kituo cha Real Madrid katika hatua za mwisho kumilisha usajili