Tuesday, September 17, 2013

Mourinho: Sitoongeza mchezaji Januari

Mourinho: Sitoongeza mchezaji Januari
KOCHA Mkuu wa Chelsea, Jose Mourinho amesema kwamba anafurahi kwa kuwa na kikosi imara.
Kutokana na kuwa na kikosi hicho kocha huyo amesema hana mpango wa kusajili mchezaji mwingine yeyote katika usajili wa dirisha dogo la Januari.
Kocha huyo wa Stamford Bridge amesema kuwa anajisifia kuwa na kikosi imara ambacho anaamini kitamvusha vema katika mwaka ujao.
Alisema kuwa "Kikosi chake ni kizuri kwani kimekamilika kila idara na kina wachezaji wadogo hali inayonifanya niamini kwamba Januari hakuna kitakachotukuta na nimezugumza nao na kuwaambia kwamba sihitaji kuona mchezaji akitoka wala kuja hapa.
Alisema "nina mfurahia kila mchezaji na simuhitaji yeyote kujiunga nasi."
Aliongeza kuwa "Sijui kama wao nao wananifurahia, ila kwangu ninafuraha kwa sababu nina wachezaji wengi wazuri na ninafuraha hata wanapofanya vizuri au vibaya, na nimekuwa nikifanya hivyo kwa moyo mweupe." alisema Mourinho

Jnjo Shelvey: Aomba radhi mashabiki wake

Shelvey: Aomba radhi mashabiki wake
KIUNGO Jonjo Shelvey ameomba radhi kwa mashabiki wa Swansea City kutokana na klabu hiyo kutoka sare ya kufungana 2-2 dhidi ya Liverpool baada ya kusema kuwa anahitaji kwenda ‘shimoni'.
Mshambuliaji huyo aliyejiunga Swansea akitokea Liverpool katika msimu wa majira ya joto alianza kwa kuipachikia klabu yake hiyo mpya bao la kuongoza kwenye dakika ya pili.
Akizungumza na Sky Sports Shelvey alisema "nahitaji kuomba radhi kwa mashabiki wa Swansea kwa kukubali suluhu ya kuruhusu bao mbili za makosa gorini mwetu hali iliyowasaidia Liverpool kupata sare,".
Aliongeza kuwa "nilifikiria tulikuwa na uwezo wa kupachika mabao mengine zaidi ya hapo. Tulianza vizuri lakini mwisho wa siku tukajikuta tukiruhusu kufanyika kwa makosa mawili yaliyowasababisha wapinzani wetu kupoata sare.
"Nilikosa raha kwa sare hiyo, hivyo sikuhitaji kusherehekea mabao hayo kama ushindi kwa sababu nimekuwa na sifa kubwa kwa mashabiki wa Liverpool kwa kuwa nilikuwa kipenzi chao tangu nikiwa hapo.