Saturday, July 20, 2013

Liver nayo yawafumua waindonesia 2-0 angalia magoli.

Tazama magoli katika mechi ya kirafiki kati ya Man United na All Stars ya Sweeden, ambayo United ilishinda kwa mabao 5-1.

Mshambuliaji wa Simba, Marcel Boniventure akitafuta mbinu za kumtoka beki wa URA ya Uganda, Walulya Derrick.
Simba yanyofolewa sharubu U/Taifa 
TIMU ya Simba jana ilichapwa mabao 2-1 katika mechi ya kirafiki ya kimataifa dhidi ya URA ya Uganda iliyochezwa Uwanja wa Taida, jijini Dar es Salaam.
Shujaa kwa upande wa URA, alikuwa Lutimba Yayo aliyeifungia mabao yote katika dakika za 54 na 74, hivyo kuanza vema ziara yao ya mechi za kirafiki ambapo leo itacheza na Yanga.
Simba walitangulia kupata bao dakika ya saba, likifungwa na Betram Mombeki akitumia uzembe wa mabeki wa URA kukawia kuokoa mpira karibu ya lango.
Simba: Abel Dhaira, Nassor Masoud Chollo, Issa Rashid, Samuel Senkoom, Rashid Juma, Jonas Mkude, Ramadhan Singano, Wlliam Lucian, Betram Mombeki, Zahor Pazi na Marcel Boniventure.
URA: Bwete Brian, Walulya Derrick, Munaaba Allon, Owino Joseph, Mugabi Jonathan, Agaba Oscar , Feni Ali, Ngama Emmanuel, Lutinga Yayo, Kasibanto James na Mugabi Yasin.
Waganda hao leo wanashuka tena dimbani kucheza na mabingwa wa soka Tanzania Bara, Yanga kwenye Uwanja whuo wa Taifa, jijini Dar es Salaam.
Wewe ndio mchizi wetu
    Wanachama Simba wanywea kwa Rage
MWENYEKITI wa Klabu ya Simba, Ismail Aden Rage, jana aligeuka shujaa kwenye mkutano mkuu wa wanachama uliofanyika Bwalo la Maofisa wa Polisi, Oysterbay, jijini Dar es Salaam na kuhudhuriwa na zaidi ya wanachama wapatao 700.
Tofauti na dalili za awali pengine mkutano huo ungekewa na presha kubwa ya wanachama kuhoji mambo mbalimbali ya kiuongozi, mkutano huo jana uligeuka shangwe na nderemo za wanachama kiasi cha kubariki kila walichoelezwa. Wakizungumza kwa nyakati tofauti kwenye mkutano huo, wanachama wengi walionesha kuridhishwa na utendaji mzima wa kiongozi wao licha ya kuwepo changamoto mbali mbali pia wanastahili kuupongeza uongozi uliopo madarakani chini ya Rage.Baadhi ya wanachama wameomba mabadiliko mbali mbali katika utendaji wa klabu wakiamini klabu hiyo chini ya Rage, watapata mafanikio makubwa katika msimu ujao.Jambo jingine ni wanachama kuombwa kuzika tofauti zilizojitokeza hadi kuibua mgogoro ndani ya klabu hiyo kiasi cha viongozi kujikuta wakigongana wao kwa wao hivyo timu kushindwa kufanya vizuri.
Akizungumza kwenye mkutano huo, Rage alisema hatarajii mapinduzi katika uongozi wake kwani wamekuwa wakichapa kazi kwa mujibu wa katiba  ya klabu hiyo, hivyo msimu ujao utakuwa ni wa mafanikio kwa klabu hiyo.
“Naaamini mambo yatakwenda vizri katika msimu ujao wa ligi na timu itafanya vizuri kutokana na mipango na mikakati tuliyojiwekeza,” alisema Rage na kuongeza wataitisha mkutano mwingine kabla ya Novemba na kuongeza:
“Tunataka tuwe na sera bora za utawala na utendaji ambapo kupitia sera hizi kutakuwa na mfumo bora wa utendaji, kiutawala, kimajukumu na kiuwajibikaji ambapo kila mtu atajikuta anafanya kazi yake,” alisema Rage.
Rage pia amesisitiza msimamo wa kulifuta tawi la Mpira Pesa kwa hoja  wanachama wa tawi hilo wamekuwa wakienda kinyume na taratibu za klabu hiyo wakitaka kuwa juu ya uongozi na kusema jambo hilo halikubaliki kamwe.
“Mpira pesa hawako juu ya Klabu ya Simba, bali ndani ya klabu hiyo, hivyo hatuwezi kuvumilia kuona wanataka kukaa juu ya klabu kitaifa, suala ambalo ni kinyume na utaratibu kabisa,” alisema Rage.
Rage alibainisha kuwa uongozi uliopo madarakani utaendelea kuwajibika katika mambo yote licha ya wanachama hao kutaka kujua hatima ya nafasi ya Makamu Mwenyekiti Geofrey Nyange ‘Kaburu’ akisema nafasi hiyo imezibwa na Joseph Itang’are ‘Kinesi.’
Katika mkutano huo ulidumu kwa dakika 60, agenda zilikuwa kuthibitisha kumbukumbu ya mkutano uliopita, hotuba ya Mwenyekiti na kupokea na kujadili taarifa za kazi kutoka kamati ya utendaji.
Nyingine ni kudhibitisha hesabu za fedha zilizokagaliwa za mwaka uliotangulia, kuthibitisha taarifa za chombo cha ukaguzi na hatua zilizochukuliwa na vyombo
vya utendaji na kudhibitisha bajeti kwa mwaka ujao.
Baada ya kumalizika kwa mkutano huo majira ya saa 5 asubuhi, ndipo ukumbi ukagubikwa na shangwe za wanachama wakiupngeza uongozi wa klabu hiyo
hadi kumbeba Ragea akionekana ni shujaa.
Hitimisho hilo lilikwenda sambamba na wanachama waliohudhuria mkutano huo, kupewa tiketi ya kuingilia uwanja wa Taifa kujionea mechi ya kirafiki ya kimataifa kati ya Simba na URA ya Uganda.
Kuelekea mkutano huo, baadhi ya wanachama walikuwa wakihoji uhalali wa mkutano huo wakidai umeitishwa kinyume cha katiba na wakapanga kwenda mkutanoni kuung’oa. 
Mourinho na Terry
Mourinho amtisha Terry
NAHODHA wa Chelsea, John Terry ana kibarua kigumu cha kupigania majaaliwa yake klabuni Stamford Bridge.
Kocha mpya wa mabingwa hao wa Europa League, Jose Mourinho amemwambia nyota huyo muhimu na kiongozi wa kweli dimbani kuwa anapaswa kuthibitisha ubora wake kikosini.
Mourinho alisema: “Terry hayuko salama na mwenyewe analitambua hilo. Jambo pekee ambalo anajua liko salama ni urafiki wetu na mahusiano yetu.
“Tumezungumza kuhusu hilo na kimsingi anatambua kwa ukamilifu kabisa kwamba urafiki ni urafiki na biashara baina yetu ni jambo jingine kabisa. Hii ni biashara hivyo, ndiyo, yeye anatakiwa kuboresha kiwango na uwajibikaji wake.
“Mimi kamwe siwezi kumlinda wala kumpa upendeleo kikosini mbele ya mwingine yeyote – na analitambua hilo kwa sababu anajua asili yangu,” alisisitiza Mourinho aliyeihama Real Madrid na kurejea Chelsea.
Terry, 32, ni beki wa kati aliyebakisha miezi 12 katika mkataba wake wa sasa na klabu hiyo na Mourinho anamtaka kukabiliana vema na changamoto kuhakikisha anathibitisha ubora wake ili aweze kuambulia mkataba mpya.
Mreno huyo aliongeza: “Kutokana na muonekano wa kimwili katika ubora, Terry anahitaji kufanya kazi kwa bidii na hapaswi kupata majeruhi kwa sababu majeraha yanavunja mageuzi ya mchezaji yeyote.

“Kwangu mimi, hiyo ndiyo hatua ya msingi kwa Terry. Anapaswa kuimarisha na kuthibitisha ubora wake kama mwingine yeyote,” alisema Mourinho kwa msisitizo.
Mo Farah
Mo Farah avunja rekodi
BINGWA medali mbili za dhahabu za mashindano ya Olimpiki ya majira ya joto 2012, Mo Farah ameibuka mshindi wa pili wa mbio za Diamond League jijini hapa, huku akivunja rekodi ya mita 1,500 iliyodumu kwa miaka 28 ya mkimbiaji Steve Cram.
Farah, Mwingereza mwenye asili ya Somalia, amejiwekea rekodi ya kuwa mtu wa sita kwa kasi duniani katika umbali huo, baada ya kutumia muda wa dakika tatu na sekunde 28.81, unaomfanya kushikilia rekodi miongoni mwa wakimbiaji barani Ulaya.
Farah, bingwa wa medali za dhahabu katika mbio za mita 5,000 na 10,000 za Olimpiki ya jijini London mwaka jana, alikuwa wa pili nyuma ya Mkenya Asbel Kiprop, ambaye alikimbia muda rekodi inayoongoza duniani wa dakika 3:27.72.
“Nimeridhishwa na matokeo na kimsingi kulikuwa na ushindani mkubwa katika mchuano huu,” alisema Farah, 30, baba wa watoto wawili pacha.
Cram, aliyekuwa akishikilia rekodi ya dunia, ambaye alitumia muda wa dakika 3:29.67 ambao ni rekodi kwa wakimbiaji raia wa Uingereza iliyodumu tangu Julai 16, 1985, alikiri kushangazwa na kasi ya Farah katika mbio hizo.
Muda huo pia unaingia katika rekodi binafsi za wakimbiaji wa kudumu Sebastian Coe aliyetumia dakika 3:29.77 mwaka 1986 na Steve Ovett (3:30.77) mwaka 1983 ambao walikamata nafasi za pili na tatu miongoni mwa Waingereza kwenye mbio za mita 1,500.

Farah alikuwa katika mbio alizozichukulia kama kipimo binafsi kuelekea mbio za ubingwa wa dunia mwezi ujao jijini Moscow, ambako atakimbia kwenye mbio za mita 5,000 na 10,000. Hakuwa na matarajio yoyote kuweka rekodi ya kutazamwa.
Luis Suarez
Madrid yaiharibia Arsenal kwa Suarez
WAKATI mshambuliaji Luis Suarez akiwakabili Liverpool kufanya nao mazungumzo ya ana kwa ana kuomba ridhaa ya kuhama, imeelezwa kuwa Arsenal wanakabiliwa na vita ya pili na Real Madrid, baada ya miamba hiyo kujitosa kuwania saini ya nyota huyo.
Madrid wanajiandaa kutuma ofa ya pauni milioni 20 pamoja na mshambuliaji wake wa kimataifa wa Argentina, Gonzalo Higuain, ili kupata saini ya Suarez nyota wa kimataifa wa Uruguay.
Mfaransa anayeinoa Arsenal, Arsene Wenger, amekuwa na mawindo mawili kwa pamoja ya kuwanasa Suarez na Higuain, lakini uamuzi huo wa Madrid unaiweka Gunners katika hatari ya kuwakosa wote kwa pamoja.
Washika Bunduki hao wa London walikuwa na imani kubwa ya kufanikiwa kupata saini ya Suarez kutoka Liverpool, baada ya kuboresha ofa yao kwa nyota huyo na kufikia kitita cha pauni milioni 40.
Gunners ilikuwa ilipandisha dau hilo kutoka ofa ya awali ya pauni milioni 35   zilizokataliwa na kocha Brendan Rodgers, aliyesisitiza kuwa hayuko tayari kumuuza mtikisa mabao wake huyo mwenye umri wa miaka 30 chini ya dau la pauni mil. 55.
Tayari Gunners ilishakubali kumlipa Suarez mshahara wa pauni 120,000 kwa wiki kumng’oa mkali huyo Anfield.
Suarez, hata hivyo, anadaiwa kupendelea kutua Madrid kuliko Arsenal, akiwa na nia ya kukimbia jinamizi la matukio tata dimbani katika soka la England.
Na sasa Madrid inamthaminisha Higuain kwa dau la pauni milioni 35 baada ya kupokea ofa ya thamani hiyo kutoka Napoli, ambapo inajiona iko sahihi kuongeza dau la pauni milioni 20 kukamilisha kitita cha pauni milioni 55 zinazotakiwa na Rodgers.
Gerardo Martino ‘Tata’
Gerardo kumrithi Vilanova
KOCHA wa zamani wa timu ya taifa ya  Paraguay, Gerardo Martino ‘Tata’ anapewa nafasi kubwa ya kuziba nafasi ya Tito Vilanova, aliyejiweka kando kutokana na sababu za kiafya.
Vilanova (44), aliyekuwa ametwa nafasi hiyo baada ya kuondoka kwa Pep Guardiola, amekuwa akisumbuliwa na kansa ya koo kwa muda mrefu.
Kuna habari kuwa, Martino mwenye umri wa miaka 50, alitarajiwa kwenda nchini Hispania kwa mazungumzo ya kazi hiyo.
Martino, aliyeipa Newell's Old Boys ubingwa wa Argentina msimu uliopita, kwa sasa yupo nje ya mkataba na wakali hao.
Ni kocha mwenye rekodi ya kubeba ubingwa wa Paraguay na mwaka 2007, alitwaa tuzo ya Kocha Bora Amerika Kusini.

Kocha huyo aliyezaliwa Novemba 20, 1992, pia amewahi kufundisha Brown de Arrecifes, Platense, Instituto, Libertad, Cerro Porteño, Colón, Libertad na timu ya taifa ya Paraguay kuanzia 2006 hadi 2011.

Utd yazidi kumtolea macho Cesc Fabregas

PAMOJA na Makamu Raia wa Barcelona,  Josep Maria Bartomeu, kusema kamwe kiungo wao Cesc Fabregas hauzwi, Klabu ya Manchester United imeongeza kasi ya kumngoa Santiago Bernabeu.
Kocha wa United, David Moyes, aliyasema hayo jana baada ya timu yake kushinda 5-1 katika mechi ya kirafiki dhidi ya A-League All Stars.
Alitumia nafasi hiyo kusisitiza kuwa, United imewasilisha ofa ya pauni mil 30, hivyo wanasubiri jibu kutoka Barcelona.
Wakati United ikiwa na mipango hiyo, nyota wake mahiri Robin van Persie, alisema jana anamkaribisha Fabregas kwa mikono mwili.
“Ni mchezaji mzuri,” alisema Fabregas alipozungumza na Channel Seven, licha ya kukiri hajawahi kuzungumza naye.