Thursday, September 19, 2013

Real Madrid kuwatoa Khedira Benzema ili wampate Aguero

Real Madrid kuwatoa Sami Khedira,
Karim Benzema ili wampate Aguero
KLABU ya Real Madrid imepanga kuto ofa kwa wachezaji Karim Benzema na Sami Khedira kwa ajili ya kumchukua Sergio Aguero wa Manchester City.
Real Madrid imepanga kuwatoa sadaka wachezaji hao kwa mpigo kwa ajili ya kubadilishana na mchezaji wa Manchester City Sergio Aguero.
Akizungumzia hilo katika mtandao wa Daily Star, klabu hiyo inayoshiriki Ligi kuu ya La Liga imedhamiria kumtwaa Aguero kwa kuwatoa wakali wao, Karim Benzema na Sami Khedira.
Benzema ametajwa kutakiwa pia na Arsenal katika kipindi cha kiangazi Klabu ya Arsenal ambayo imeandaa dau la Euro milioni 40.

Nicky Butt amkaribisha Scholes United

Nicky Butt amkaribisha Scholes United
Scholes wa mbele kushoto akiwa kwenye benchi la ufundi

KOCHA wa timu ya vijana Nicky Butt, amemkaribisha Paul Scholes kama kocha msaidizi katika klabu ya Manchester United.
Wachezaji hao maswahiba ambao waliwahi kucheza pamoja katika klabu hiyo.
Butt amemkaribisha Scholes, kwa klabu yake ya vijana kuichapa ile ya Bayer Leverkusen kwa bao 4-3 katika mechi ya kuwania kombe la vijana la UEFA.
Wakati klabu hiyo ikifanya mauaji hayo Scholes(38), alikuwa benchi.
Akimzungumzia mchezaji huyo Butt alisema katika televisheni ya MUTV kuwa "amestaafu soka kwa sasa lakini mtu kama Schole ni muhimu kwa United ambao wameamua kumrejesha katika njia ya kunisaidia.
"Nashukuru kwa Veterani huyu kuja kuungana na klabu hii kwa ajili ya kuinua vipaji vya vijana wa hapa na ninaamini kwa kushirikiana naye tutainua vipaji vingi.
"Ni muhimu kwa ajili yetu kwani atakuwa akionekana katika klabu hii kwa namna anavyokuwa anahitaji."