Thursday, July 25, 2013

Hawa ni Samurai wanaoichezea Arsenal
Samurai Podolski na Mertesacker
Mertesacker na Podolski
Big Four kwa mtindo wa NYEUSIIIIII
BAADHI timu kubwa zinanazo shiriki Ligi Kuu England maarufu kama 'Big four' zikiwamo Mabingwa wa England, Manchester United, Manchester City na Chelsea zimejikuta zikiangukia kwenye jezi aina moja zenye rangi nyeusi. Jezi hizo watazitumia katika mechi za ugenini tu, ziangalie kwenye picha hapo chini baadhi ya wachezaji wamezivaa kwa ajili ya kuzitambulisha.
Man United
Man City
Chelsea

Guardiola awapiga wanae 2-0
Baadhi ya wachezaji wa Bayern wakinyanyua kombe
KOCHA Mkuu wa Bayern Munich Pep Guardiola ameifunga klabu yake ya zamani Barcelona kwa ushindi wa goli 2-0 katika mechi ya kirafiki iliyopigwa ndani ya dimba la Allianz Arena, jijini Munich.
Philipp Lahm ndiye aliyefungua kalamu ya mabao hayo katika dakika ya 14 goli hilo lililodumu kwa muda mrefu mpaka ilipofika dakika 87 Mshambuliaji wao hatari Mario Mandzukic akashindilia msumari wa mwisho.
Timu hizo hii ndiyo mechi yao ya kwanza tangu walipokutana kwenye mchezo wa nusu fainali ya Kombe la Mabingwa wa Ulaya, ambao mechi hiyo Barcelona walikubali kipigo cha Mbwa Mwizi cha mabao 7-0.

Azam kukipiga na 'vigogo' Sauzi
Wachezaji wa Azam FC wakishangilia moja ya mechi zao
KLABU inayokuja kwa kasi katika medani ya soka hapa nchini, Azam FC, inatarajiwa kucheza mechi nne za kirafiki katika ziara yao nchini Arika Kusini ikiwamo dhidi ya mabingwa wa nchi hiyo, Orando Pirates.
Azam FC, klabu inayozipa changamoto klabu kongwe za Simba na Yanga kutokana na uimara wake kila idara, tofauti na wakongwe hao wanaojiendesha kwa kuunga kuunga.
Meneja wa Azam FC, Said Jemedari, alisema kila kitu hadi sasa kinakwenda sawa na inasubiriwa siku ya kukwea pipa kwenda kufanya ziara yao, ambayo itakuwa na manufaa kwa timu nzima ambayo inakabiliwa na michuano mbalimbali hapo mbeleni.
Jemedari alizitaja timu ambazo wataumana nazo katika ziara yao ya siku 12 kuwa ni Amazulu, Supersport United, Bidvpst Wits pamoja na Orando.
“Tuna imani mechi hizo nne zitamuonyesha mwalimu wapi tuendako na kujua makosa ya kufanyia maboresho kabla ya mchezo wetu na Yanga Agosti 17 na Ligi Kuu,” alisema Jemedari.
Katika hatua nyingine, Jemedari alisema juzi walishuka dimbani kumenyana na Kombaini ya Majeshi, mchezo uliopigwa dimba la Chamazi nje kidogo ya jiji na kumalizika kwa sare ya bao 1-1, mabao yalifungwa na Hussein Nyamandulu wa CISM na Tchetche Kipre kwa Azam FC.
CISM inaundwa na wachezaji wa timu za Jeshi ambazo ni JKT Ruvu, Mgambo, Ruvu Shooting, Oljoro, Trans Camp, Kipanga na Rhino Rangers ipo katika maandalizi ya kushiriki mashindano hayo yatakayorindima kuanzia timu za Majeshi Afrika Mashariki yatakayofanyika Agosti 5-17 jijini Nairobi nchini Kenya.
Man City wampa kiwewe Mourinho
Jose Mourinho
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema Manchester City watakuwa washindani wakubwa katika Ligi Kuu
hasa baada ya kufanya usajili wa nguvu chini ya kocha mpya, Manuel Pellegrini.
Kauli ya Mourinho, inatokana na Man City kutumia gharama kubwa kuwasajili nyota kadhaa kama Alvaro Negredo, Stevan Jovetic na Jesus Navas.
Pamoja na usajili huo, Mourinho anaamini Manchester City walipaswa kufanya kwanza  tathmini ya usajili wa msimu uliopita.
City imetumia kiasi cha pauni mil 100 kupata saini ya Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk, Jesus Navas na Alvaro Negredo kutoka Sevilla na Stevan Jovetic kutoka Montenegro.
Mourinho aliyerejea Chelsea akitokea Real Madrid, amesema kwa usajili huo, Man City watakuwa washindani wakubwa msimu ujao.
Alipoulizwa juu ya kumwania Wayne Rooney, alisema hawezi kusema lolote.