Thursday, August 22, 2013

Bale muda si mrefu kutua Real Madrid

Bale muda si mrefu kutua Real Madrid

KLABU ya Real Madrid imekaribia kumng’oa Gareth Bale kutoka klabu ya Tottenham hadi Santiago Bernabeu pamoja na Franco Baldini aliyetua White Hart Lane katika msimu huu.
Kuna habari kuwa, Mkurugenzi wa Spurs, ameweka sharti la kutaka mpango huo umhusishe Fabio Coentrao wa Real Madrid huku ikielezwa ndani ya saa 24, kila kitu  kitakuwa kimefahamika.
Kama Real Madid itafanikiwa kumtwaa Bale, itakuwa ni kutimia kwa ndoto ya muda mrefu
ya klabu hiyo ambapo uhamisho wake ukitarajiwa kuwa si chini ya pauni mil 80.

Rooney azikutanisha Man United, Chelsea

Rooney azikutanisha Man United, Chelsea
JAPO Kocha wa Manchester United, David Moyes amekuwa akisema Wayne Rooney hatoki Old Trafford, viongozi wa klabu hiyo wameanza mazungumzo na Chelsea.
Yaelezwa mpango huo unakwenda pamoja na Juan Mata kwenda Old Trafford kama Rooney atakwenda Stamford Bridge.
Nje ya Mata, mazungumzo yamejikita kwenye thamani ya Rooney kutokana na United kutaka pauni mil 40 huku Chelsea ikiwa tayari kwa pauni mil 28.
Mpango huo unafanyika wakati ambapo Kocha wa Chelsea, Jose Mourinho akisema  bado anahitaji mshambuliaji, iwe kutoka Old Trafford au kwingineko.