Thursday, July 25, 2013

Man City wampa kiwewe Mourinho
Jose Mourinho
KOCHA wa Chelsea, Jose Mourinho amesema Manchester City watakuwa washindani wakubwa katika Ligi Kuu
hasa baada ya kufanya usajili wa nguvu chini ya kocha mpya, Manuel Pellegrini.
Kauli ya Mourinho, inatokana na Man City kutumia gharama kubwa kuwasajili nyota kadhaa kama Alvaro Negredo, Stevan Jovetic na Jesus Navas.
Pamoja na usajili huo, Mourinho anaamini Manchester City walipaswa kufanya kwanza  tathmini ya usajili wa msimu uliopita.
City imetumia kiasi cha pauni mil 100 kupata saini ya Fernandinho kutoka Shakhtar Donetsk, Jesus Navas na Alvaro Negredo kutoka Sevilla na Stevan Jovetic kutoka Montenegro.
Mourinho aliyerejea Chelsea akitokea Real Madrid, amesema kwa usajili huo, Man City watakuwa washindani wakubwa msimu ujao.
Alipoulizwa juu ya kumwania Wayne Rooney, alisema hawezi kusema lolote.

No comments:

Post a Comment