Azam Tv yawachanganya Yanga
SAKATA la Klabu ya Yanga kugomea udhamini wa Azam Tv katika
Ligi Kuu Tanzania bara, limezidi kupata nguvu baada ya viongozi wa matawi ya
klabu hiyo kubariki msimamo huo wa uongozi.
Msimamo huo ulitolewa jana na viongozi wa matawi ya klabu hiyo jijini Dar es Salaam ambao walikutana kujadili
suala hilo na kusema wanaunga mkono.
Akizungumza kwa niaba ya wenzake, Bakili Makele alisema
viongozi wao (Yanga) wapo sahihi kujitoa kwenye udhamini huo na kusema wanapata
shaka na uharaka ya Kamati ya Ligi katika suala hilo.
Bakili alisema licha ya kutowekwa kwa tenda ya suala hili ili kushindaniwa katika mazingira ya wazi, pia jambo hilo
lingeachwa lishughulikiwe baada ya uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la soka la
Tanzania (TFF).
Kutokana na dosari hizo, wanachama hao wamemsihi Rais wa
TFF, Leodegar Chilla Tenga kuingilia kati na kusema wanahofia jambo hilo
limeharakishwa kwa maslahi binafsi.
“Jamani tamko letu ni kwamba, tunaungana na viongozi wetu,
kwani Yanga ndio kila kitu hapa nchini, Na Azam Tv, inataka kutuchanganya,”
alisema Bakili.
Hata hiyo Makele alionekama kutoa kauli zenye mwelekeo wa
wivu wa maendeleo kwa kusema kitendo cha Azam Tv kumiliki haki za Ligi Kuu,
kutainufaisha klabu ya Azam.
“Jamani, kitendo cha Azam TV kumiliki haki za Ligi Kuu,
kutaifanya timu yao izidi kupata kipato, hivyo ving’amuzi vyao tusinunue,”
alisema Makele na kuikiwa na viongozi wenzake wa matawi ….Yanga Oyeeeee.
Mwandishi Wetu ilipomtafuta Katibu Mkuu wa klabu hiyo
Laurance Mwalusako ni kwanini walikubali
jambo likiwa kwenye mchakato, alisema walijaribu bila mafanikio.
“Ni kweli kwenye vikao tulikuwepo, lakini hatukuafiki kabisa
na ndio maana nikasubiri tulifikishe kwa kamati ya utendaji ili wafanye,”
alisema Mwalusako.
Kauli hiyo ya Mwalusako imekuja kutokana na wadau kuhoji mantiki ya klabu hiyo kupinga suala hilo wakati Yanga
iliwakislishwa na yeye Mwalusako na Makamu Mwenyekiti, Clement Sanga.
“Sisi tuliomba kuona mkataba kwanza, ili tujue haki na mambo
katika mkataba huo, lakini TFF ilikagoma
kwa kusema yatosha kusomewa.
Alipotafutwa Mwenyekiti wa Kamati ya Ligi, Wallace Karia
kuhusu msimamo huo wa wanachama, alisema hawana muda kuzozana wanasubiri
kufanyia kazi taarifa rasmi itakayofika kwao.
“Yanga ilikuwa na wajumbe wake katika mchakato mzima wa jambo hili, hivyo
hatuoni tija kurumbana nao katika kipindi hiki. Kama kweli wamegomea, watuarifu
rasmi kwa maandishi.
No comments:
Post a Comment